This article has been published in Enabling Education Review 2
Click here for publication table of content

Reference:

Link: https://www.eenet.org.uk/enabling-education-review/enabling-education-review-2/eer-2-swahili-translation/2-16/

Machapisho muhimu

Vipeperushi na mabango

Kila mtoto anahitaji mwalimu anayejali mjumuisho na aliyesomea vizuri IDDC, 2013 
Hiki ni kipeperushi cha A4 chenye pande mbili kilichotayarishwa na IDDC na EENET kama marejeo ya haraka kuhusu elimu ya ualimu na mjumuisho, kwa ajili ya matumizi wakati wa Kampeni ya Kimataifa ya Elimu mwaka 2013. Mchoro uliopo katika kipeperushi hiki umeingizwa katika jarida hili. Kipeperushi hiki kinapatikana katika lugha za Kiingereza, Kiarabu, Kifaransa, Kihispania na Kijerumani. Kinapatikana katika mtandao: http://bit.ly/1cmb25L

Walimu kwa Wote: Ufundishaji jumuishi kwa ajili ya watoto wenye ulemavu, IDDC, 2013 
Karatasi hii ya sera inaambatana na kipeperushi cha IDDC . Inatoa habari zaidi juu ya hali ya sasa ya ufundishaji na mafunzo na inatoa mapendekezo ya kina zaidi juu ya hatua za kuchukuliwa katika kuandaa walimu ambao wataweza kuwajumuisha watoto wenye ulemavu katika madarasa ya kawaida. Inapatikana katika mtandao: http://bit.ly/1glgWuQ

Videos

Watoto viziwi na vijana duniani kote mara nyingi huyimwa haki yao ya elimu, (Human Right Watch, 2013). 
Video hii inayochukua muda mfupi inaonesha umuhimu wa kuwawezesha watoto viziwi kujifunza kupitia katika lugha ya alama. Iangalie katika mtandao: http://bit.ly/1bT5ODw

Miongozo

Kukuza elimu mjumuisho ya ualimu: Mwongozo wa Utetezi, UNESCO, 2013
Hii ni seti ya vijitabu vitano inayolenga kumsaidia mtu yeyote anayetaka kushiriki katika utetezi kuhakikisha kwamba mafunzo ya ualimu ya kabla ya kuingia kazini yanawaandaa vizuri walimu kwa ajili ya elimu mjumuisho . Vijitabu vyenyewe ni: Utangulizi, Sera, Zana/Vifaa, Mtaala na Mbinu. Kila kijitabu ni rahisi, kinachukua muda mfupi kukisoma, na kinaweza kusomwa peke yake au kusomwa kama sehemu ya seti nzima. Inapatikana katika mtandao: http://bit.ly/1hJIcDG

Elimu Mjumuisho: Utangulizi
Leonard Cheshire Disability, 2013. 

Hiki ni kijitabu kidogo kinachoangalia mbinu za Leonard Cheshire Disability za elimu mjumuisho na kinatoa baadhi ya mifano kutoka katika juhudi zake kote duniani. Kinapatikana katika mtandao: http://bit.ly/1glgZ9T

Ripoti

Haki Sawa. Fursa Sawa. Elimu kwa watoto wenye ulemavu,
Kampeni ya Kimataifa kwa ajili ya Elimu, 2013

Ripoti hii ni hati ya maandalizi kwa ajili ya Wiki ya Vitendo ya Kimatifa 2014. Inaangalia hali ya elimu kwa watoto wenye ulemavu na inapendekeza mikakati na hatua imara za utetezi na kukuza mjumuisho. Inapatikana katika mtandao: http://bit.ly/1bbAZ78

 

Mtandao wa Kuwezesha Elimu (Pasifika EENET)

EENET Pasifika logo

Huu ni mtandao mpya wa kupashana habari wenye lengo la kuongeza maarifa na ufahamu kuhusu elimu mjumuisho. Una uhusiano wa karibu, ingawa hauendeshwi, na EENET.

Pasifika EENET ni matokeo ya utafiti wa Dk Susie Miles (Chuo Kikuu cha Manchester);
Sekretarieti ya Jukwaa la Visiwa vya Pasifiki; na kuwashirikisha wadau katika visiwa vya Cook, Fiji, Kiribati na Samoa. Utafiti huu uliwasikiliza watoto, wazazi, watu wenye ulemavu, walimu, wakufunzi wa walimu na watunga sera katika kutambua mitandao na namna ya kutoa kipaumbele kwa habari.

Tovuti ya Pasifika EENET ilizinduliwa na Pacific Islands Forum Secretariat (Sekretarieti ya Jukwaa la Visiwa vya Pasifiki) mnamo mwezi wa Septemba 2013. Angalia: www.eenetpasifika.org or email: eenetpasifika@gmail.com