This article has been published in Enabling Education 8
Click here for publication table of content

Reference:

Link: https://www.eenet.org.uk/enabling-education-review/enabling-education-8/newsletter-8-kiswahili-translation/mtazamo-wa-sera-lugha-na-ujumuishaji-lao-pdr/

Mtazamo wa Sera: Lugha na Ujumuishaji, Lao PDR

Anupam Ahuja

Nchini Lao PDR watoto wanafundishwa kwa lugha rasmi, Kilao, kuanzia shule ya msingi. Hata hivyo asili mia arobaini na tatu ya watoto wa shule wanajifundisha kuongea, kusoma na kuandika Kilao kama lugha ya pili. Wanafunzi hawa wako katika upungufu mkubwa na wakati mwingine huwa na shida iliyokithiri ya lugha inayochangia kutoendelea na masomo. Matarajio madogo, ubaguzi, na ukosaji wa mfano bora wa kuiga na marika wa kitamaduni ina maana kwamba watoto ambao hawaongei Kilao kama lugha yao ya kwanza ndio sana wanaweza kuacha kuendelea na masomo. Anupam Ahuja anaonyesha uhusiano baina ya kutengwa kilugha na kutofaulu shuleni, na anaelezea maarifa za serikali ya Lao kushughulikia jambo hili.

Ili kuendeleza Kilao kama lugha ya taifa, sera za elimu zinahitaji kuitumia kama njia ya kufundishia shuleni. Hii ni shida sana kwa maana kuna lugha themanini na mbili zinazotambulika rasmi nchini Lao PDR na lafidhi nyingi tofauti tofauti. Zote ni lugha zinazotumika, lakini si zote zinazo maandishi.

Ijapokuwa sheria inasema kwamba lugha za wachache zaweza kutumika kwa kufundishia, kwa kweli lugha ya Kilao ndiyo inatumika. Kufundisha lugha ya mama ni ngumu, kwa sababu haiko dhahiri ni lugha gani zitumiwe.

Hesabu zinaonyesha kwamba watoto wasioweza kuongea Kilao vizuri ndio hushindwa na masomo mapema. Hili ni sababisho mojawapo la kiwango kikubwa cha watoto kuacha shule na kurudia madarasa hasa kwa daraja ya kwanza na ya pili katika shule za msingi. Hii inathibitisha kuwa ghali kwa wizara ya elimu, kwa sababu kiwango kikubwa cha wanaorudia ina maana kuwa malipo ya elimu itakuwa juu. Maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya nchi yanahasirika na haki za watu wachache hazishuhulikiwi. Uamuzi wa kufaa ili kupunguza shida ya ndani ya sera hii inahitaji kubuniwa.

Shida za lugha zifanywa kubwa sana kwa njia za kitamaduni za kufundishia. Walimu wengi wana kiwango kadiri cha kuelewa jinsi watoto hukuza lugha na kujua kusoma, na namna ya kupanga shughuli muhimu za utumizi wa kugha. Utaratibu wa mafunzo na vitabu vya mafundisho hulenga utamaduni wa mkondo wa kawaida na lugha. Mabadiliko yanaendelea, lakini njia ya kuridhisha na nyenye fikra pana inabuniwa.

Wizara ya elimu inachukuwa hatua mwafaka ili kupunguza matokeo mabaya ya sera, na kuimarisha na kukuza lugha ya taifa. Walimu wana:

  • wekwa tayari kutumia utaratibu unaofaa kufundisha Kilao.
  • tayarishwa kuleta lugha katika maisha kwa kupanga mazingira ya madarasa ili watoto waongee, wasome na kuandika kuhusu vitu wanavyovijua.
  • himizwa kutumi vitu tofauti tofauti vya kusaidia kufundishia na kusomea (mfano picha, vitu vya kuona na vya kutumia sehemu za mwili .) ili kutoa maana kwa lugha iliyotumika.
  • pewa mafunzo ya kufunza kwa uhodari na kwa wepesi, ambapo inaruhusu watoto kuunganisha kile wanaona na kusikia pamoja na kile wanajua- muhimu kwa kuendeleza lugha.
  • jifunza kwamba kazi kwa vikundi vidogo inaenda sambamba na kusoma kichangamfu.

Hadithi ya Vieng

“Ni msichana mwenye haya kwa sababu ya mdomo wake wa upande na anaonekana ana matatizo ya kusoma”, walisisitiza walimu wanne wa kwanza. “Vieng anaongea Kihmong nyumbani. Hajui sana Kilao. Anaona haya kutoka nje- ni mdomo wake wa upande”.Mama yake Vieng aliniambia.

Nilipouliza kama kuna mtu anaweza kuongea Kihmong, wasichana wawili na kijana mmoja wakajitokeza mbele. Niliwauliza wanisaidie kufundisha darasa jinsi ya kuhesabu na lugha ya Kihmong. Tulisema nambari kwa Kilao na kwa Kihmon. Niliangalia upande wa Vieng. Ghafla aliketi wima na kuungana nasi – alichanuka mfano wa nyunginyungi kwenye kidibwi cha maji.

  • Nilipokuwa nikienda, niliongea na walimu wake kuhusu kuwatia watoto wake moyo ili kufundishana wao kwa wao mambo mengine na nyimbo kwa Kkilao, Kihmong na Kikhmu. “Unafikiria Vieng ni akili punguani?” Mwalimu mmoja aliniuliza. Nilibadilisha lugha kwa ghafla kutoka Kilao hadi Kihindi na nikapayuka kwa muda wa dakika moja. Hawakunielewa. “Unaongea lugha geni kwake” Nikasema

“Mnaweza kuwahimiza watoto wa Hmong kusaidia kila mmoja kujifundisha maneno fulani ya Kihmong?” Niliuliza mwalimu mkuu. Alikubali, lakini aliniangalia kwa kushangaa. Atakuwa anavunja sheria.

Dkt. Anupam Ahuja ni mshauri wa kufanya kazi apendapo na anauzoefu wa zaidi ya miaka ishirini katika nyanja ya elimu na uangalifu kwa kustawisha uchumi kwa pamoja. Amefanya kazi kwa kiwango cha taifa na cha kimataifa katika Afrika na bara Asia na anaweza kufikiwa kwa:

A-59 Malviya Nagar
New Delhi – 10 017
India
Tel: +91 11 26681303
Mobile: +9810652249
Fax: +91 11 24362798
Email: ahujaa@vsnl.net