This article has been published in Enabling Education 8
Click here for publication table of content

Reference:

Link: https://www.eenet.org.uk/enabling-education-review/enabling-education-8/newsletter-8-kiswahili-translation/elimu-ya-mjumuisho-na-uhusikaji-wa-wazazi-mongolia/

Elimu ya mjumuisho na uhusikaji wa wazazi Mongolia

Mongolia na elimu ya mahitaji maalum
Mongolia iko katikati ya kitovu cha Asia ya kati, katikati ya Uchina na Urusi. Idadi yake ya watu milioni 2.6 imeenea hapa na pale. Nchi imegawanywa katika mikoa ishirini na moja na manisipaa moja ambayo imegawanywa katika tarafa tisa. Mongolia ni kadiri ya nchi ndogo yenye asili mia 30.7 ya idadi ya watoto walio kati ya miaka 0-14.

Kabla ya mwaka 1989, serikali ya ujamaa ya Mongolia ilianzisha sera ya kuwaweka pamoja watu walemavu kwa kuwajengea jarifa za shule maalum na mahala pa kutunzwa. Huku njia hii ikishughulikia mahitaji muhimu ya walemavu, iliwatenga na maisha ya kijamii na ya kisiasa. Kufuatia mabadiliko ya kisiasa na ya kiuchumi ya miaka ya 1990, muundo huu wa kuwaweka walemavu pamoja ulianguka. Kutokana na ukosefu wa pesa na raslimali, shule maalum mashambani zilifungwa na manufaa ya kijamii kwa watoto walemavu zilipungua sana.

Muundo wa elimu ya lazima umedhoofika kuto kipindi cha mabadiliko, na watoto walemavu sasa wamekuwa wengi kati ya wale wanaoacha shule. Watoto walemavu wana fursa ndogo ya kupata elimu,hasa sehemu za mashambani. Shule chache za elimu maalum ziko kwa watoto wenye shida ya kusikia,kuongea na upungufu wa akili. Shule kama hizi zapatikana katika mji mkuu, Ulaanbastar. Moja pekee ndio inatoa mafunzo kwa watoto wasioona.

Shida zinazowakabili watoto walemavu.

  • Watoto 527,000 wako katika shule za upili, kati ya hawa, 40,000 ni walemavu na asili mia 0.38 wako katika shule maalum.
  • Asili mia 10.3 ya watoto wenye umri kati ya miaka 8-10 ambao wanastahili kusoma shuleni, na asili mia 66.6 ya watoto wadogo, hawawezi kupata mahitaji ya kusomea.
  • Asili mia 7.1 ya watoto wanaosoma mashuleni ni walemavu.
  • Asili mia 11.6 ya watoto ambao wanastahili kusoma mashuleni hawawezi kwenda kwa sababu ya uzito wa ulemavu, kama ilivyosemwa katika sehemu ya mwisho katika utafiti kutoka kitengo cha elimu mjumuisho ya wizara ya elimu

Kulingana na waashiria wa elimu,Mongolia ni nchi yenye wasomi wengi ambao asili mia 98.5 ya idadi yake ya watu wanaweza kusoma na kuandika. Ubaguzi wa jinsia katika elimu iko chini sana na kuna asili mia kubwa ya watoto walemavu katika shule za kawaida kuliko nchi zingine. Walakini, elimu mara nyingi haileti faida, na ufikiaji mbaya kwa watoto walemavu. Mara nyingi utaratibu wa mafunzo hauwezi badilika sambamba kwa watoto walemavu,na walimu hawana ufahamu mwema wa mahitaji ya watoto walemavu, ama uwezo wao. Walimu wengine wana hali ya ubaguzi kwa watoto walemavu,ambao mara nyingi hawatambulikani kwa sababu ya ukubwa wa madarasa. Watoto wengi wenye ulemavu mkubwa bado wako nyumbani.

Elimu mjumuisho

Mwanzo wa elimu ya mjumuisho Mongolia ilihusika kwa karibu na mradi wa kipekee wa mahitaji ya elimu wa DANIDA, 1994-1998, iliyofanywa katika mikoa mitatu na kwa shule mbili katika mji mkuu. Mradi wa Okoa Watoto UK’s (SC UK) (1998 hadi sasa) kwa kujumuisha watoto walemavu kwa shule za kawaida za mwanzo, na hivi majuzi kwa shule za msingi, ilifanyika kwa mikoa mitatu.

Kufanikiwa kwa kuendeleza miradi ya elimu ya mjumuisho kunahitaji uhusishaji na usaidizi wa wazazi wa watoto walemavu katika daraja zote. Kuanzia mwaka wa 1998, kwa usaidizi wa mradi wa kuokoa watoto (SC UK), vikundi vya familia zenye watoto walemavu waliunda chama kisichosajiliwa ambacho kilikuwa kimehusishwa karibu sana na SC UK katika kuanzisha shughuli za elimu ya mjumuisho kwao. Kufikia mwaka wa 2000, kikundi hiki kisicho na utaratibu kiliendelea mpaka kikasajiliwa kama shirika lisilo la serikali -muungano wa wazazi wenye watoto walemavu iliyohusika na kutetea haki, na kutoa usaidizi kwa, watoto walemavu.

Wakati wa karakana ya kimataifa kuhusu sera za elimu mjumuisho kwa watoto walemavu, iliyofanyika Ulaanbaatar mnamo machi 2003, neno ‘elimu mchanganyiko’ ilibadilishwa kuwa ‘elimu mjumuisho’ kwa maoni ya mradi wa kuokoa watoto [sc uk] mkurugenzi wa utaratibu Mongolia, Bw.Karlo puskarica.

Karakana iliyosimamiwa na mradi wa watoto [sc uk] ulilenga: kuipa sura mpya uanzilishi wa elimu mjumuisho Mongolia; kusaidia wahusika kusaidiana , na kujifundisha kutoka, nchi zingine kuhusu maendeleo na utekelezaji wa sera; kutambua mambo muhimu na mapendekezo ya kuendeleza na kutekeleza sera hizi Mongolia. Mradi wa kuokoa watoto [sc uk] unaamini kwamba kuhimiza sera ndio njia ya kusuluhisha matatizo.

Wizara ya elimu imefanya mabadiliko katika muundo wake na kuimarisha kitengo cha elimu mjumuisho (IEU) kupitia usaidizi wa kifundi na kifedha kutoka kwa SC UK.

Ushirikiano

SC UK una ushirikiano thabiti na muungano wa wazazi wenye watoto walemavu [APDC], na, kupitia ushirikiano na IEU, utaratibu wa elimu mjumuisho kwa watoto walemavu unabuniwa. Hii ilikubaliwa kwa pamoja na waziri wa elimu, waziri wa afya na waziri wa maswala ya jamii na uchumi mnamo Disemba 2003. Kwa sasa wizara hizi,mradi wa kuokoa watoto [sc uk], APDC na vyama vingine vyenye uhusiano vimeunda kamati tekelezi ya kuangalia utekelezaji wa mradi.

Umuhimu wa kuhusika kwa wazazi

Wazazi wanaamini kuhusika kwao na sauti yao ni kiungo muhimu katika kutekeleza elimu mjumuisho. APDC ina uwezo wa kusaidia katika uendelezaji wa huduma zaidi za elimu na kuinua hali ya kuishi ya watoto wao. Ni kutekeleza mradi wa APDC wa kuwapa kupanua tasisi unaosimamiwa kifedha na shirika la wazungu (European union) na SC UK.

Mafanikio ya APDC ni pamoja na: uhusiano wa kimataifa na usambazaji habari, uendelezaji wa mashirika, mwelekeo na muundo. La muhimi sana ni kwamba, imeunganisha zaidi ya wazazi 700. Hii imepaza sauti ya watoto walemavu na kuwa changamoto kwa watu kujua haki zao.

Hivi majuzi tulipata fursa ya kutembelea shirika la kuwezesha elimu kote [EENET] nchini Uingereza kama moja wapo ya kujifunza katika ziara yetu. Tulimkuta Susie Miles, ambaye alitupatia mawazo mengi kuhusu elimu mjumuisho. Habari ni muhimu kwa wazazi, kwa vyama vingine vinavyohusiana, na kwa watu wote kwa jumla. Kubadilishana maoni na maarifa na nchi zingine kuhusu elimu mjumuisho ni muhimu kwa nchi inayoendelea kama Mongolia.

Hitimisho.

Kila mtoto ana haki ya kupata elimu. Kila mtoto angependa kwenda shule ya watoto wadogo na shule yenyewe,lakini kwa sasa sio kila mtoto ana fursa hii. Tunaamini elimu mjumuisho ndio njia mwafaka ya kufuata ili kutimiza haki ya kila mtoto ya kupata elimu.Hatua ya kwanza kwa elimu mjumuisho inajengwa nchini mwetu, kwa usaidizi wa sehemu zote za jamii: watoto, wazazi, na hata pia mashirika ya serikali na yasiyokuwa ya serikali.

Shirika la wazazi wenye watoto walemavu linatazamia kuwasiliana na kupeana mawazo na maoni na washiriki wengine wa EENET kote ulimwenguni.

N.Enkhtsetseg
Chief Executive Officer
Association of Parent’s with Disabled Children
5-52, Diplomatic Compound, 6th khoroo,
Chingeltei District, Ulaanbaatar, Mongolia
POB: 460, 46A
Tel: +(97611) 318 060
Fax: +(97611) 327 391
Email: apdc@mongol.net

Kwa uhusiano na mradi wa kuokoa watoto [Sc Uk], serikali imehusika na mambo kadhaa ya utaratibu wa ‘mjumuisho’ kama vile kuungana na watoto wa kuranda randa mitaani, walioacha shule, na familia zilizoathiriwa na umaskini na familia zilizovunjika. Kitengo cha elimu mjumuisho ya wizara ya elimu [MOE] ina mtazamo mkubwa, ambao unahusisha watoto wa kuranda randa mitaani na vikundi vingine ambavyo havijabahatika kiuchumi. Muungano wa wazazi wenye watoto walemavu [APDC] hushirikiana na watoto walemavu, hivyo basi hauko peke yake. Nilikuwa mshauri kwa muungano wa wazazi wenye watoto walemavu [APDC] kutoka mwanzo na nimefurahishwa na kazi yao na vile wamejitoa mhanga katika kuendeleza utaratibu. Wafanyi kazi wakuu wana moyo na ni wenye bidii. Kwa kifupi wameweza kubuni shirika ambalo ni la Demokrasia kwa muundo na kinahusisha wazazi na watoto kwa jumla katika kutoa sauti katika kila pembe ya Mongolia. Peter Blackley, Mshauri wa kuendeleza chama kisichosajiliwa.

“Asante sana kwa kutukubalia chuo kikuu cha Manchester…..imetupatia wazo la maana sana. Vigitabu vyenu na mtandao ndio chanzo kikubwa cha habari kwa mambo yanayo wahusu watoto walemavu na inasaidia sana kazi yetu…. Naweza sema kwamba EENET ni rasli-mali muhimu ya habari na ninaweza iita “Uchumi Mzuri wa Busara.”

N Enkhtsetseg