1
00:00:02,000 --> 00:00:06,000
Mambo yanayochangia ujumuishwaji katika ya makuzi ya awali ya mtoto na elimu

2
00:00:06,000 --> 00:00:13,760
Umuhimu wa makuzi ya awali na elimu kwa mtoto

3
00:00:23,700 --> 00:00:29,060
Elimu na makuzi ya awali ya mtoto yana umuhimu wa kipekee. 

4
00:00:29,760 --> 00:00:34,000
Watoto huanza kujifunza kabla hata hawajazaliwa. 

5
00:00:37,080 --> 00:00:48,000
Mbinu tunazotumia kuwasaidia watoto katika makuzi na kujifunza katika umri wao wa utotoni huathiri makuzi na uwezo wao wa kujifunza baadaye. 

6
00:00:50,000 --> 00:00:57,000
Wazazi na walezi wangependa watoto wao wakue vyema. 

7
00:00:57,000 --> 00:01:05,000
Wanapenda kuhakikisha kuwa watoto wanapata fursa ya kukua, kujifunza na kufikia ukomo wa vipaji vyao. 

8
00:01:06,000 --> 00:01:13,000
Watoto wanahitaji kusaidiwa kufikia hili. 

9
00:01:17,000 --> 00:01:25,200
Makuzi ya awali na mazingira ya kutolea elimu yana mchango mkubwa katika kukuza fursa hizi. 

10
00:01:28,500 --> 00:01:33,480
Mataifa mbalimbali duniani yamejiwekea malengo kama kuridhia mikataba mbalimbali 

11
00:01:33,480 --> 00:01:39,680
– kama vile Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa, Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Watu wenye Ulemavu na Mkataba wa Haki za Mtoto – 

12
00:01:39,680 --> 00:01:49,600
 ili kuhakikisha kwamba makuzi ya awali na elimu yanapatikana kwa watoto wote wa kiume na kike tena katika mazingira jumuishi.

13
00:01:51,000 --> 00:02:01,000
Watoto wote – wa kike na kiume, bila ya kujali utaifa wao, lugha, dini, ulemavu, akiwa mkimbizi au katika hali nyengine yoyote – 

14
00:02:01,000 --> 00:02:06,000
wanapaswa kupata elimu pamoja katika jamii zao.  



15
00:02:06,000 --> 00:02:15,000
Kuna aina tofauti za makuzi ya awali ya mtoto, malezi na elimu. Majina tofauti hutumiwa kuelezea.  



16
00:02:15,000 --> 00:02:22,960
Katika jamii yako inawezekana unafahamu kuhusu ‘kindergarten’ (maandalizi), ‘nursery’ (maandalizi), ‘playgroup’ (vikundi vya kucheza), ‘pre-school’ (shule za awali), 

17
00:02:22,960 --> 00:02:30,600
‘early learning centre’ (vituo vya awali vya kujifunzia), ‘daycare’ (kituo cha kulelea Watoto cha kutwa), ‘childcare’ (malezi ya watoto)na majina mengine. 

18
00:02:30,600 --> 00:02:39,480
Kwa jina lolote litakalotumika, mazingira yote ya kujifunzia lazima yawe jumuishi.

19
00:02:45,000 --> 00:02:51,440
Katika video ifuatayo utajifunza njia rahisi ambazo walimu, 

20
00:02:51,440 --> 00:02:59,140
katika mazingira yoyote, wanaweza kuimarisha utendaji wao wa kila siku na kuwa jumuishi zaidi.

21
00:03:09,080 --> 00:03:16,400
Je! Ni sifa zipi zinazotambulisha makuzi ya awali na elimu jumuishi kwa mtoto? 

22
00:03:21,500 --> 00:03:30,000
Elimu na makuzi jumuishi ya awali yanawawezesha watoto wote kujifunza pamoja na wenzao – tangu wakiwa na umri mdogo. 

23
00:03:30,000 --> 00:03:35,000
Ikimaanisha kwamba wanajifunza kupokea na kuthamini uanuai (utofauti) wakiwa bado katika umri mdogo, 

24
00:03:35,400 --> 00:03:41,000
jambo ambalo linasaidia kuweka misingi ya uanzishwaji wa jamii jumuishi.

25
00:03:41,000 --> 00:03:51,200
Ndio maana ni muhimu kwa walimu wanaosomesha watoto katika madarasa ya awali kutambua na kuhamasisha uanuai.

26
00:03:51,700 --> 00:04:00,200
Watoto hunufaika kwa namna tofauti kupitia uzoefu wa kusoma pamoja katika vikundi jumuishi (anuai).

27
00:04:02,840 --> 00:04:12,200
Kuna faida kubwa kwa watoto kusoma wakiwa katika vikundi. Wanapokua katika vikundi, hujitahidi kusaidiana.

28
00:04:12,200 --> 00:04:24,200
Hushikana na kuwa mfano wa matofali ambayo yanaungana na kujenga jengo moja. 

29
00:04:35,800 --> 00:04:44,900
Familia yetu inafurahia masomo ya awali. Lee Ann amefurahi. 

30
00:04:44,900 --> 00:04:55,900
Sasa hivi ana marafiki na anacheza na watoto wengine badala ya kushinda nyumbani kila siku. 

31
00:05:01,640 --> 00:05:10,900
Napenda vikao vya asubuhi vikiwa ni sehemu ya ratiba yetu, na tunajitahidi kuviendesha kila siku. 

32
00:05:10,900 --> 00:05:22,900
Lengo la vikao vya asubuhi ni kumsaidia kila mtoto kujisikia huru, mwenye kuthaminiwa, muhimu na anaekubalika.

33
00:05:32,900 --> 00:05:44,900
Ubora wa huduma jumuishi za elimu na makuzi ya awali ya mtoto ndio chanzo cha mafanikio kwa kila kitu.  

34
00:05:52,440 --> 00:06:00,000
Tunajifunza kwa kucheza na watoto. Ukitaka kuwafundisha watoto, unapaswa kwanza kujua jinsi ya kucheza nao. 


35
00:06:00,000 --> 00:06:03,000
Watoto hujifunza kwa kucheza. 

36
00:06:03,000 --> 00:06:07,600
Kucheza ndio njia bora zaidi kwa watoto kukua na kujifunza. 

37
00:06:07,600 --> 00:06:11,720
Ndio maana ni muhimu kwa walimu wa shule za awali 

38
00:06:11,720 --> 00:06:18,420
kujua jinsi ya kuongoza na kurahisisha mchakato wa kujifunza kwa watoto pamoja na kukuza ujuzi wao kupitia michezo.

39
00:06:20,300 --> 00:06:28,500
Shule za maandalizi ni kwa ajili ya kucheza. Tunawafundisha watoto kwa kucheza nao.  

40
00:06:28,500 --> 00:06:34,200
Ijapokua wanacheza, bado huwa wanajifunza kupitia kucheza. 

41
00:06:35,200 --> 00:06:42,800
Wanapocheza watoto hujumuika pamoja, wanadadisi (tafiti). Kupitia michezo, hujifunza mazingira yanayowazunguka.

42
00:06:42,800 --> 00:06:47,450
Na mwalimu huwa mwenzao wanaecheza nae pamoja. 

43
00:06:50,250 --> 00:06:56,280
Wanapocheza hujumuika pamoja na kupata fursa ya kujuana vizuri, wanajifunza kujumuika. 

44
00:06:56,280 --> 00:07:07,000
Pia huimarika zaidi kimwili. Kucheza ni njia bora inayowafanya wawe na afya.  


45
00:07:07,000 --> 00:07:12,640
Ndio maana ni muhimu kuwapatia muda wa kutosha wa kucheza. Wanapocheza pamoja huwasiliana. 


46
00:07:12,640 --> 00:07:20,000
Hujumuika, wanajifunza kushirikiana, hujifunza haya pamoja. 

47
00:07:20,000 --> 00:07:28,920
Kushirikiana katika kila walichonacho, tabia ambayo ni muhimu kadiri wanavyokua. 

48
00:07:37,000 --> 00:07:41,520
Elimu na makuzi ya awali jumuishi – ambayo yamejikita katika michezo – 

49
00:07:41,520 --> 00:07:49,520
hujenga msingi imara wa kufurahia kujifunza katika maisha yote. 

50
00:07:55,100 --> 00:08:05,000
Unapofundisha japo kitu kidogo tu, ujuwe kuwa unajenga msingi. Huwezi tu kujenga nyumba bila ya msingi. 

51
00:08:08,600 --> 00:08:13,520
Kujenga uhusiano baina ya maisha ya nyumbani, maisha binafsi, jamii na mazingira ya kujifunzia 

52
00:08:13,520 --> 00:08:24,000
ni mbinu muhimu wanayoitumia walimu wa shule za awali katika kujenga shauku ya mtoto kujifunza. 

53
00:08:24,000 --> 00:08:30,600
Walimu wa shule za awali hulenga katika kuvumbua vitu ambavyo mtoto anavipenda ili wakuze ubunifu wao na udadisi – 

54
00:08:30,600 --> 00:08:38,520
vipawa ambavyo vitawasaidia watoto kadiri wanavyokua.

55
00:08:54,520 --> 00:09:00,220
Walimu wa shule za awali pia husaidia ustawi wa kimwili na kihisia

56
00:09:00,220 --> 00:09:07,000
afya na usalama wa watoto wote walio chini ya uangalizi wao. 

57
00:09:16,390 --> 00:09:26,500
Mambo gani yanapaswa kuepukwa katika elimu na makuzi ya awali ya mtoto?

58
00:09:27,400 --> 00:09:32,800
Elimu katika makuzi ya awali ni zaidi ya kumuandaa mtoto kwa elimu ya msingi. 

59
00:09:32,800 --> 00:09:40,600
Tunaweza kuona kuwa katika muktadha fulani elimu katika makuzi ya awali haihamasishi mjumuiko (uanuwai), 

60
00:09:40,600 --> 00:09:50,840
haijikiti katika burudani na michezo, haijengi misingi ya kufurahia kujifunza. 

61
00:09:50,840 --> 00:10:00,000
Haitoi fursa ya mtoto kukua kihisia au kujenga shauku endelevu ya kujifunza. 

62
00:10:00,000 --> 00:10:08,960
Watoto wadogo wanaweza kusomeshwa katika makundi makubwa kwa kutumia mbinu zinazotumika kuwasomeshea watoto wakubwa. 

63
00:10:08,960 --> 00:10:19,360
Baadhi ya programu za elimu ya awali hujaribu kuwaandaa watoto kwa kuwafundisha masomo ya elimu ya msingi kama vile kusoma na hisabati. 

64
00:10:19,360 --> 00:10:25,260
Hata wazazi wanaweza kupendelea jambo hili kwa watoto wao lakini sio sahihi kwa watoto wa rika hili na itapelekea, 

65
00:10:25,260 --> 00:10:34,480
kwa mfano, watoto kupoteza kipindi muhimu cha maisha yao ya kujifunza na kukua kwa kucheza na kutafiti.  



66
00:10:34,480 --> 00:10:39,440
Hizi ni stadi za msingi zinazowaandaa watoto kwa maisha yao ya shule. 

67
00:10:39,440 --> 00:10:48,400
Kuna ushahidi kwamba kuwaanzisha mapema watoto masomo ya shule hakuwafanyi wawe katika nafasi maalumu ya kufanikiwa. 

68
00:10:48,400 --> 00:10:54,200
Sio jumuishi kwa sababu inalazimisha uwepo wa matumaini makubwa 

69
00:10:54,200 --> 00:10:59,200
kwa watoto ambao wanatofautiana mno. 

70
00:10:59,200 --> 00:11:05,480
 Kwa hivyo iwapo tunataka kuhakikisha uwepo wa elimu mjumuisho 

71
00:11:05,480 --> 00:11:11,000
katika elimu ya awali tunapaswa kuepuka mbinu ya kuwafundisha kwa kuwahutubia. 

72
00:11:11,000 --> 00:11:18,480
Tunapaswa kuepuka kugeuza elimu ya awali kuwa elimu rasmi.  

73
00:11:44,400 --> 00:11:46,480
UFANYE NINI?

74
00:11:46,480 --> 00:11:52,980
Shirikiana na walimu wengine katika elimu mjumuisho

75
00:11:54,980 --> 00:12:02,600
Kila mwalimu wa shule ya awali anapaswa kujifunza kuhusu misingi na matendo ya ujumuishwaji. 

76
00:12:02,600 --> 00:12:07,920
Hili linaweza kufanyika kupitia warsha za mafunzo au kupitia programu 

77
00:12:07,980 --> 00:12:12,720
 za kujisomea mwenyewe! 

78
00:12:14,000 --> 00:12:20,280
Unaweza pia kujifunza mengi kuhusu ujumuishwaji kwa mwenzako.

79
00:12:22,380 --> 00:12:32,200
Mwalimu mpya anapojiunga na shule yetu ya maandalizi, tunamfundisha kuwa kujifunza hakuwezi kuwa jambo lenye kuchosha. 

80
00:12:32,200 --> 00:12:41,000
Kwa mfano, iwapo watakua wanafundisha kuhusu mti, hawatakiwi kusimama tu karibu ya mti na kutoa maelezo kuhusu mti.  

81
00:12:41,000 --> 00:12:47,840
Badala yake, watoto wanapaswa kujumuika na huo mti; wanaweza kuupima, kucheza mchezo wakitumia majani yake. 

82
00:12:47,840 --> 00:12:51,650
Mchakato mzima wa kujifunza lazima uambatane na kucheza.

83
00:12:51,650 --> 00:13:03,650
Kwa namna hii inakua rahisi kwa watoto na walimu pia, na inaleta raha zaidi kuliko kukaa na kusikiliza maelezo.

84
00:13:08,000 --> 00:13:13,960
Mnaweza kuwa na mwenzenu katika shule yenu ambaye ana uzoefu na watoto, 

85
00:13:13,960 --> 00:13:19,100
au ana uzoefu wa kuwafundisha watoto wenye ulemavu. 

86
00:13:19,100 --> 00:13:26,560
Unaweza kuwataka ushauri juu ya namna bora ya kuwasaidia watoto katika darasa lako. 

87
00:13:26,560 --> 00:13:34,200
Lakini usiweke matarajio kwa mwenzenu mwenye tahasusi maalumu ya utaalamu kuchukua jukumu la kukufundishia wanafunzi wako. 

88
00:13:34,200 --> 00:13:40,500
Bado litabaki kuwa jukumu lako kuwasaidia wanafunzi wako kukua na kujifunza.

89
00:13:45,580 --> 00:13:53,000
Utakaposhirkiana na walimu wengine kama timu, unaweza kuelezea wasiwasi wako, ukatoa mawazo yako na uzoefu wako pia. 

90
00:13:53,000 --> 00:13:57,640
Hii itakusaidia kutatua kwa usahihi shida yoyote utayoipata 

91
00:13:57,640 --> 00:14:03,540
katika kuwalea na kuwafundisha watoto.

92
00:14:11,940 --> 00:14:19,240
Huwa tunakutana mara kwa mara kujadili malengo yetu na kuandika mpango wa maendeleo wa kila mtoto. 

93
00:14:19,240 --> 00:14:27,440
Tunaweka malengo kwa kila mtoto na kila baada ya miezi mitatu, au hata chini ya hapo, huwa tunakutana kutathmini tulipofikia kuelekea kutimiza malengo, 

94
00:14:27,440 --> 00:14:34,000
 iwapo tumetoa mafunzo sahihi kwa kutumia mbinu sahihi za kusaidia ukuaji wa mtoto. 

95
00:14:34,000 --> 00:14:39,940
Wakati mwengine lengo halikua sahihi, tunapaswa kubadili.

96
00:14:50,160 --> 00:14:58,840
Kikawaida, mazingira ya shule za awali huwa sio rasmi sana ukilinganisha na msingi au sekondari.

97
00:14:58,840 --> 00:15:04,160
Hii itakupa wewe, na walimu unaofanya kazi nao pamoja, fursa zaidi ya kuamua jinsi ya kuratibu 

98
00:15:04,160 --> 00:15:11,060
na kutekeleza mchakato wa kujifunza kwa watoto, na jinsi ya kutatua changamoto za ujumuishwaji. 

99
00:15:11,060 --> 00:15:16,800
Kwa mfano,unaweza kutumia mbinu ya kufundisha kwa timu, ili uweze kushirikiana na wenzako 

100
00:15:16,800 --> 00:15:22,280
kupanga na kutekeleza shughuli za kujifunza.  



101
00:15:28,000 --> 00:15:33,320
Na unaweza kuvikusanya vikundi tofauti vya watoto kwa ajili ya kushiriki katika mazoezi tofauti. 

102
00:15:33,320 --> 00:15:41,440
Hapa, watoto kutoka shule ya awali na kutoka sekondari wanashiriki katika mazoezi pamoja 

103
00:15:41,440 --> 00:15:47,320
wakiburudika na kusoma pamoja.

104
00:15:58,720 --> 00:16:08,040
Tambua mahitaji ya kila mtoto katika makuzi

105
00:16:14,400 --> 00:16:22,880
Walimu wa shule za awali wanahitaji kuwa na uelewa wa msingi wa makuzi ya kijamii, kimwili, kiakili, 

106
00:16:22,880 --> 00:16:27,880
mawasiliano na kihisia ya mtoto. 

107
00:16:27,880 --> 00:16:36,000
Kila mtoto hukua katika hatua za kipekee, kwa hivyo ufuatiliaji wa mara kwa mara unapaswa kufanyika kwa kila mtoto. 

108
00:16:36,000 --> 00:16:41,800
Unapaswa kuwafuatilia watoto ili ufahamu na kufuatilia makuzi ya mtoto mmoja mmoja, 

109
00:16:41,800 --> 00:16:46,000
vitu wanavyovipenda, uwezo, na mahitaji yao. 

110
00:16:46,000 --> 00:16:52,240
Hii isihusishe kumlinganisha mtoto mmoja na mwengine. 

111
00:16:53,040 --> 00:16:59,680
Mimi hufuatilia watoto ili kutathmini nini wanakijua na vipi wanaendelea. 

112
00:16:59,680 --> 00:17:04,680
Tutapoanza kutumia mbinu mpya za kufundishia, tunaangalia mabadiliko ya darasani na 

113
00:17:04,680 --> 00:17:11,000
iwapo watoto wanaipenda na wanajifunza vyema kwa mbinu mpya. 

114
00:17:11,000 --> 00:17:21,500
Pia hua tunafuatilia kwa hivyo tunaweza kutambua vipaji na uwezo wa watoto.

115
00:17:28,000 --> 00:17:37,000
Unapaswa kubaini iwapo ukuaji wa vipaji fulani vya mtoto ni wa taratibu, haraka zaidi au tofauti na ulivyotarajiwa. 

116
00:17:37,000 --> 00:17:42,960
Hatimaye unaweza kuchagua mbinu za kufundishia na kujifunzia kulingana na mahitaji ya mtoto. 

117
00:17:43,000 --> 00:17:49,080
Unaweza pia kuwaomba wazazi wa mtoto au walezi, na hata walimu wengine wenye ujuzi maalumu, 

118
00:17:49,080 --> 00:17:54,730
kukusaidia katika kuchagua mbinu za kufundisha ama kujifunzia kwa mtoto.  

119
00:17:59,200 --> 00:18:04,280
Kutoa usaidizi wa mapema kwa mtoto kutazuia uwezekano wa kuchelewa 

120
00:18:04,280 --> 00:18:08,500
kwa makuzi kuwa na athari kubwa kadiri ya siku zinavyopita.

121
00:18:08,500 --> 00:18:15,480
Unaweza kugundua pale watoto watapohitaji usaidizi wa marekebisho au huduma za afya. 

122
00:18:15,480 --> 00:18:21,960
Huhitaji kuwa mtabibu, lakini unaweza kushirikiana na watoa huduma wengine 

123
00:18:21,960 --> 00:18:27,760
kubaini mahitaji ya mtoto na kuyashughulikia.

124
00:18:35,000 --> 00:18:44,680
Leo nipo na mama yake Lee nikifuatilia maendeleo yake. Kwanza tulimtambua mtoto na kumtathmini

125
00:18:44,680 --> 00:18:51,680
afya yake na uwezo wake kimwili. Baadaye tukashirikiana na timu ya wataalamu kutoka Cape Town. 

126
00:18:51,680 --> 00:19:01,700
Walimtengenezea kiti cha magurudumu.Baadaye tulikirekebisha kwa mujibu wa hali ya mtoto. Sasa hivi mtoto yupo shule.


127
00:19:30,500 --> 00:19:35,900
Kuna taratibu za kawaida tu ambazo unaweza kuzifuata ili kubaini maendeleo ya makuzi ya mtoto.

128
00:19:35,900 --> 00:19:43,280
Unaweza kuangalia matendo ya mtoto, ishara katika uso wake, viashiria vya vitendo anavyovitumia kuelezea hisia zake na tabia.

129
00:19:43,280 --> 00:19:52,500
Kufuatilia uwezo wao wa kuwasiliana wanapozungumza na kujumuika na watoto wengine.

130
00:19:53,000 --> 00:19:59,500
Watazame wakiwa peke yao, wawili wawili na katika vikundi..

131
00:20:06,240 --> 00:20:18,200
Watazame watoto wakifanya mambo mbalimbali yanayoakisi uwezo wao wa kijamii, kimwili, kiakili, kuwasiliana, na kihisia.

132
00:20:18,200 --> 00:20:28,440
Unaweza kugundua ni kipi kinamvutia mtoto au kipi hakimpendezi.

133
00:20:28,440 --> 00:20:35,700
Watazame jinsi wanavyojumuika na watu wazima na watoto wakubwa.

134
00:20:37,280 --> 00:21:47,200
Na ungana nao kwa kucheza nao au kuzungumza. 

135
00:21:52,700 --> 00:22:00,480
Unapaswa kujenga uhusiano baina ya mafunzo unayoyatoa na maisha binafsi ya mtoto na nyumbani kwao. 

136
00:22:03,000 --> 00:22:13,200
Toa mifano ya desturi, lugha, michezo, matukio, watu na vitu ambavyo mtoto anavijua pale nyumbani kwao.

137
00:22:13,200 --> 00:22:19,680
Ili kufanikisha hili, shirikiana kwa karibu na wazazi na walezi. Wao ni wataalamu. 

138
00:22:19,680 --> 00:22:26,360
Wanamjua mtoto wao vizuri zaidi kuliko mtu mwengine yeyote. 

139
00:22:32,000 --> 00:22:35,720
Watakuambia ni vitu gani mtoto anavijua sana pale nyumbani. 

140
00:22:35,720 --> 00:22:44,520
Wewe pamoja na wao mnaweza kujuzana kuhusu vitu anavyovipenda mtoto, maendeleo yake na changamoto. 

141
00:22:49,840 --> 00:23:00,000
Nimefarijika juu ya uhusiano uliopo baina ya walimu wa shule ya awali na mimi mwenyewe kama mzazi. 

142
00:23:00,000 --> 00:23:06,280
Huwa nawaeleza kinachotendeka nyumbani, hali ya Illia, na, wao pia, 

143
00:23:06,280 --> 00:23:11,720
hunieleza kuhusu kilichotokea shule, amejifunza nini, tulenge katika jambo gani

144
00:23:11,720 --> 00:23:18,360
na kwa pamoja tunasaidia katika makuzi ya mtoto.

145
00:23:29,400 --> 00:23:37,880
Bila ya shaka, baadhi ya wazazi huomba ushauri, kwa mfano, “Nifanyeje niwapo nyumbani kumsaidia mtoto katika eneo fulani?” 

146
00:23:37,880 --> 00:23:49,300
Tunajadili na kuzungumza kila kitu: tufanye nini, turatibu vipi kazi zao wawapo nyumbani, jinsi ya kumuanzisha mtoto katika jambo fulani. 

147
00:23:51,000 --> 00:23:55,160
Wewe na wenzako mnaweza kuwahamasisha wazazi na walezi kushiriki kikamilifu  

148
00:23:55,160 --> 00:24:00,000
katika makuzi na mafunzo ya mtoto wao kwa kuyafanya mazingira ya kusomea kuwa jumuishi 

149
00:24:00,000 --> 00:24:05,600
na rafiki kwa wazazi na walezi. 

150
00:24:06,200 --> 00:24:14,000
Unaweza kutoa fursa ya wao kushiriki katika harakati za masomo, kujifunza na kujadiliana hapo shule.  


151
00:24:14,000 --> 00:24:19,000
Ni muhimu pia uwe unafuatilia na kuwasiliana na familia. 

152
00:24:19,000 --> 00:24:27,200
Wewe na wenzako mnaweza pia kuzuru nyumbani kwa mtoto ili kufahamu zaidi kipi kinasaidia au kukwaza makuzi 

153
00:24:27,200 --> 00:24:36,080
ya mtoto na juhudi zake za kujifunza nyumbani kwao, au ni kipi kinawazuia wasihudhurie au kushiriki darasani kwako au katika kikundi.

154
00:24:49,500 --> 00:24:54,080
Kuna hali tofauti za maisha, familia tofauti. 

155
00:24:54,080 --> 00:25:01,300
Kila mmoja hufika shule asubuhi akitokea nyumbani akiwa na matatizo binafsi au furaha. 

156
00:25:01,300 --> 00:25:10,120
Mara zote huwa tunaafikiana: wazazi, watoto na sisi walimu hushirikiana pamoja kama timu. 

157
00:25:10,120 --> 00:25:18,200
Wakati mwengine inakupasa kushirikiana na walezi ambao sio wanafamilia, ili kujua mazingira ya mtoto ya nyumbani. 

158
00:25:18,200 --> 00:25:25,250
Watoto ambao hawaishi na familia zao hukabiliana na vikwazo vya ziada vinayokwaza ujumuishwaji katika harakati zao za kujifunza.

159
00:25:25,250 --> 00:25:36,880
Nafanya kazi hapa katika kituo cha kulelea watoto cha Nqaba Yethu nikiwa msimamizi wa kituo. Tuna watoto 15. Tunasajili aina zote za watoto. 

160
00:25:36,880 --> 00:25:43,680
Tunajaribu kuwaleta pamoja na kuwafanya wajisikie wapo nyumbani. Watoto wengi tulionao hapa, 

161
00:25:43,680 --> 00:25:48,680
inawabidi kuanza shule za awali ambazo ni muhimu kwa kila mtoto. 

162
00:25:48,680 --> 00:25:56,680
Tunajaribu kuhudhuria shule kila siku, ili kuwasiliana kwa karibu na mwalimu na kufahamu kinachosumbua. 

163
00:25:56,680 --> 00:26:00,480
Inawezekana wakati mwengine ikachukua muda mrefu kidogo kwa mtoto [kujifunza] 

164
00:26:00,480 --> 00:26:10,080
ikimaanisha kwamba kuna mengi zaidi unayopaswa kuyafanya ukishirikiana na mtoto katika kazi zake za shule.

165
00:26:15,560 --> 00:26:25,400
Jenga mazingira rafiki, yanayochochea kujifunza

166
00:26:26,320 --> 00:26:32,040
Mazingira jumuishi ya makuzi ya awali yanapaswa kuwa rafiki, 

167
00:26:32,040 --> 00:26:37,040
yenye kuburudisha, na yanayochochea hamu na furaha ya kujifunza. 

168
00:26:37,040 --> 00:26:44,040
Ukiwa ni mwalimu wa shule jumuishi za awali, kuna mengi unayoweza kuyafanya ili kufanikisha hili. 

169
00:26:44,040 --> 00:26:54,540
Kwa mfano:Pangilia vizuri eneo la kufundishia ili kila sehemu iweze kutumika kwa shughuli tofauti za kujifunzia.

170
00:26:57,080 --> 00:27:03,560
Wakati wa mchana, watoto wanaweza kuzunguka bila pingamizi na kufanya vitu tofauti katika sehemu tofauti. 

171
00:27:03,560 --> 00:27:12,100
Wanaweza kufanya kazi zao wakiwa wameketi kwenye madawati au wanaweza kukaa kwenye mkeka au sehemu nyengine.

172
00:27:16,000 --> 00:27:24,760
Tumia mazingira ya nje kwa kujifunza kupitia michezo, na kwa watoto kupumzika na kufurahi.

173
00:27:28,000 --> 00:27:35,300
Tenga eneo ambalo utaweka aina fulani ya vitu vya kuchezea na kujifunzia. 

174
00:27:35,300 --> 00:27:38,900
Hakikisha unavipanga vizuri vitu vyote. 

175
00:27:38,900 --> 00:27:48,600
Kupangilia vyema kila kitu kunasaidia watoto wajisikie huru, kujiamini, na kujifunza wanapohitaji kitu waende wapi au wakachukue wapi.

176
00:27:48,600 --> 00:27:55,440
Andaa utaratibu tofauti wa kukaa, ili kuwawezesha watoto kuchagua pa kukaa kama ni sakafuni au kwenye meza, 

177
00:27:55,440 --> 00:28:03,880
au juu ya viti wakiwa kwenye vikundi na rafiki zao, popote pale itapokuwa rahisi na faraja kwao.

178
00:28:05,900 --> 00:28:11,960
Wakati mwengine, vipindi vya elimu na makuzi ya awali huendeshwa katika mazingira ya muda kama

179
00:28:11,960 --> 00:28:21,110
mikutano za kijiji, au katika miundombinu ya muda mfupi kama vile kambi za wakimbizi. 

180
00:28:21,110 --> 00:28:33,110
Lakini bado unaweza kubuni njia nyengine za kujenga mazingira ambayo ni jumuishi, yenye kuburudisha, yenye kuchangamsha na yenye kupendeza kwa watoto katika kila kipindi. 

181
00:28:33,410 --> 00:28:41,200
Panga siku yako na tofautisha baina ya vipindi vya masomo na mazoezi

182
00:28:43,000 --> 00:28:47,200
Ratiba ni muhimu kwa watoto wadogo. 

183
00:28:47,200 --> 00:28:55,280
Kuwa na utaratibu unaotabirika huwasaidia kujisikia wana amani. 

184
00:28:56,400 --> 00:29:03,280
Ukiwa ni mwalimu wa shule jumuishi ya awali, unapaswa kujipanga vyema ili vipindi vya masomo

185
00:29:03,280 --> 00:29:11,350
na pia mazingira yanayozunguka yasiwe ya fujo na yenye kuwachanganya watoto. 

186
00:29:13,800 --> 00:29:19,520
Ratiba isiyo nyumbulifu haina ulazima wala sio sahihi. 

187
00:29:19,520 --> 00:29:26,900
Lakini unaweza kupanga ni muda gani watoto watatoka nje na muda gani wa kuwepo ndani, na pia nyakati za chakula. 

188
00:29:26,900 --> 00:29:35,850
Na utapaswa kuhakikisha kuwa siku nzima wana fursa za kucheza aina tofauti za michezo. 

189
00:29:35,850 --> 00:29:47,000
Katika shule yetu ya awali, na labda hata shule nyengine, kuna aina fulani ya ratiba ya kila siku. Baada ya mazoezi, wanakunywa chai. 

190
00:29:47,000 --> 00:29:54,800
Vipindi vya masomo vinatofautiana na vinabadilika; tunajaribu kuvifanya viwe vinaburudisha. 

191
00:29:54,800 --> 00:30:01,800
Tunatumia visaidizi vingi ili kuwafanya watoto wavutiwe zaidi.

192
00:30:01,800 --> 00:30:14,340
Unapaswa pia kuweka bayana matarajio yako kwa watoto, ili wajue ni jambo gani wanaruhusiwa kufanya na jambo gani hawaruhusiwi kufanya.

193
00:30:16,040 --> 00:30:19,840
Hakikisha masomo yote yanaongozwa na michezo. 

194
00:30:19,840 --> 00:30:28,600
Wape watoto nafasi ya kuamua wanataka kucheza mchezo gani au wanataka kutumia au kuchezea vifaa gani.

195
00:30:28,600 --> 00:30:38,480
Pale watoto watapokua na fursa ya kufanya mambo yanayohusu michezo kwa kutumia vitu wanavyovipenda, watakua na umakini zaidi

196
00:30:40,500 --> 00:30:49,340
Harakati hizo pia zitawasaidia kukuza vipawa fulani, kama vile kuhesabu. 

197
00:30:49,340 --> 00:30:54,040
Tunajua kwamba watoto wanatofautiana katika kujifunza. 

198
00:30:54,040 --> 00:31:03,000
Baadhi yao hujifunza kwa haraka unapowaimbia, unapotumia nyimbo, au mashairi, wengine hujifunza kwa haraka wanapoona kitu. 

199
00:31:03,000 --> 00:31:08,560
Wengine hujifunza kwa haraka wanapochezea kitu kwa mikono yao. 

200
00:31:08,560 --> 00:31:20,560
Ndio maana tunahakikisha tunafanya kila kitu ili tuweze kumfikia kila mtoto kulingana na tofauti aliyonayo katika kujifunza. 

201
00:31:29,360 --> 00:31:33,080
Bila shaka tunatumia mikabala inayotofautiana. 

202
00:31:33,080 --> 00:31:39,880
Mwalimu anapoandaa somo, wanapaswa kuzingatia kwamba kuna mtoto mwenye mahitaji maalumu, 

203
00:31:39,880 --> 00:31:46,380
na mchakato wa kujifunza unapaswa kuzingatia uhitaji wa huyo mtoto. 

204
00:31:49,580 --> 00:31:56,280
Wape watoto nafasi ya kuamua kasi ya kujifunza – iwapo wanataka kufanya kitu kwa haraka na ukakamavu, 

205
00:31:56,280 --> 00:32:02,480
au taratibu na kwa utulivu; iwapo wanataka wafanye wakiwa kimya  au wapige kelele.

206
00:32:04,000 --> 00:32:12,900
Waache wakamilishe wanachokifanya – usiwaharakishe ili wapate kufanya kitu chengine.

207
00:32:14,800 --> 00:32:28,920
Watoto watapokuwa na nafasi ya kuamua namna na kasi ya kujifunza kwa njia ya kucheza, kile wanachofanya huwa rahisi kwao na huendana na mahitaji na uwezo wao.

208
00:32:28,920 --> 00:32:35,320
Wakati mwengine unaweza kutaka kuwahimiza watoto wachangamke au wawe watulivu. 

209
00:32:35,320 --> 00:32:42,000
Mazoezi yanayohusisha muziki na harakati yanaweza kusaidia.

210
00:32:42,000 --> 00:32:55,360
Unapaswa kuhakikisha kwamba watoto wanashiriki kikamilifu katika kila kipindi. 

211
00:32:56,100 --> 00:33:06,000
Tumia vifaa halisi kuchochea hamasa ya kujifunza 

212
00:33:10,400 --> 00:33:20,000
Watoto wadogo hufahamu kwa urahisi pale panapokuwa na uhusiano baina ya wanachojifunza na maisha halisi. 

213
00:33:22,700 --> 00:33:28,600
Tunajaribu kuhakikisha tuna michezo ya nje ya darasa. 

214
00:33:28,600 --> 00:33:36,240
Tuna eneo zuri nje ya madarasa lenye mimea na miti, ambayo huwapa watoto fursa tofauti za kujifunza. 

215
00:33:36,240 --> 00:33:48,150
Tunawasaidia kujifunza.Tuna mazingira ya kubuni ambapo watoto wanaweza kujifunza kwa kusimama katika sehemu mbalimbali na kufanya mambo tofauti

216
00:33:48,150 --> 00:33:59,040
kama vile michezo, burudani, tafiti, uchunguzi, kusaka utajiri, na mazoezi mengine ya kutumia akili. 

217
00:33:59,040 --> 00:34:10,000
Kwa namna hii, huzunguka katika mazingira haya ya kubuni na kujfunza mambo mbalimbali yanayohusu mazingira na vitu. 

218
00:34:15,000 --> 00:34:25,480
Tunatumia baadhi ya vitu tunavyoviokota nje au chochote kile. Katika shule za awali unakisanifu ili kiweze kutumika.

219
00:34:27,720 --> 00:34:37,590
Katika shule yetu ya awali hapa hatuna vifaa vya kujifunzia lakini huzunguka nikikusanya chochote nikipatacho nje 

220
00:34:37,590 --> 00:34:44,560
na huvitumia kutengeneza wanasesere na baadae tunawatumia kuchezea.

221
00:34:44,560 --> 00:34:51,800
Tunakusanya changarawe na watoto wanapochezea huwasaidia kujifunza nambari.

222
00:34:51,800 --> 00:35:04,800
Katika shule za awali, tunapocheza nje, tunatumia matairi yaliyokwishatumika. Watoto wanapenda kusukuma na kuyabiringisha. 

223
00:35:10,240 --> 00:35:26,800
Ukiwa ni mwalimu wa shule jumuishi ya awali, unapaswa kuwapatia watoto vifaa halisi ili wavitumie siku nzima.

224
00:35:34,000 --> 00:35:47,800
Kutumia vifaa kama hivi kutawasaidia watoto wadogo kujifunza rangi, maumbo, mguso, harufu, sauti, na uzito. 

225
00:35:49,600 --> 00:35:59,080
Vitu vyenye hisia tofauti ni muhimu sana kwa wanafunzi wenye changamoto ya kuona na kusikia.

226
00:35:59,080 --> 00:36:06,400
Vitu vya kugusa na kusanifika vikiwa ni sehemu ya kujifunzia vinaweza kuwasaidia watoto wanaohitaji usaidizi wa viungo, 

227
00:36:06,400 --> 00:36:14,900
au wenye shida ya kufahamu na kukumbuka vitu.

228
00:36:17,900 --> 00:36:33,900
Kwa kutumia maelezo haya ya kawaida, mwalimu wa shule ya awali anaweza kufanya kazi kwa kutumia dhana ya ujumuishi na usaidizi katika utoaji wa mafunzo na makuzi ya watoto wote.
