Home learning (Swahili)

£0.00

Double-sided A2 poster.

Published by EENET and NAD, 2020

87 in stock

Category:

Description

Kujifunza hufanyika kila wakati tunaposikilizana na tunaposilikiliza mazingira yanayotuzunguka …

 • Kila mmoja husikiliza. Watu wazima husikiliza watoto, watoto husikiliza watu wazima, watu wazima husikiliza watu wazima na watoto husikiliza watoto.
 • Omba msaada unapokuwa huelewi kitu fulani. Mtu yeyote anaweza kukusaidia.
 • Simulia hadithi ukitumia ishara na ishara za uso. Hakikisha kila mtu anaweza kukuona wakati unasimulia hadithi.
 • Sikiliza vilivyo karibu na wewe – ndege, wanyama, mvua. Jaribu kutengeneza sauti zinazofanana. Kujifunza hufanyika kila wakati tunapocheza na kufurahi tukiwa peke yetu na tunapokuwa na mtu mwengine …

Kujifunza hufanyika kila wakati TUNAPOCHEZA na KUFURAHI tukiwa peke yetu na tunapokuwa na mtu mwengine …

 • Kila siku, zunguka kwa njia yoyote unayoweza. Cheza. Rukaruka. Zungukazunguka.
 • Fanya mabadiliko ya michezo ili kila mtu ajiunge nayo. Hii inaweza kuwa kubadilisha kanuni au kubadilisha harakati.
 • Tunga michezo mipya na uwafundishe wengine jinsi ya kuicheza.
  Unapokuwa peke yako, unaweza kuwa na utulivu au kushughulika sana kulingana na jinsi unavyojihisi

Kujifunza hufanyika kila wakati TUNAPODADISI na TUNAPOGUNDUA zaidi kuhusu sisi wenyewe na watu wengine …

 • Jaribu kufanya kitu kipya, hata ikiwa ni vigumu kwanza.
 • Jifunze kutoka kwa kila mmoja. Tafuta mtu anayeweza kukufundisha kitu unachotaka kujifunza.
 • Lima chakula. Tunza mti. Rekebisha kitu. Jenga kitu. Badilisha kitu.
 • Uliza maswali: Je, kwa nini hii inafanyika? Je, hii inafanyaje kazi? Je, ikiwa nitaibadilisha hii?

Kujifunza hufanyika kila wakati TUNAPOBUNI na TUNAPOUNDA kitu kwa kutumia kitu chochote kilicho karibu…

 • Tumia vitu vyovyote vilivyopo karibu, kama chupa zilizokwishatumika, pakiti, vijiti na matope kutengeneza vitu vingi tofauti. Kitu chochote kinaweza kutumika kukusaidia ujifunze.
 • Tumia mawazo yako na vitu unavyoweza kuvipata kutengeneza hadithi. Hadithi hizi zinaweza kuwa ‘halisi’ au za ‘kubuni’.
 • Fanya maigizo ya hadithi zako za kubuni. Wape wengine kile ulichokiunda. Simulia hadithi!
 • Kata herufi moja moja zilizoandikwa katika pakiti zilizokwishatumika na unda maneno.

Kujifunza hufanyika kila wakati tunapojihisi SALAMA na KUPENDWA hata wakati tunapokabiliwa na matatizo …

 • Kujihisi tuko salama na wenye kupendwa ndio msingi wa kujifunza na ukuaji. Bila ya kujihisi salama na kupendwa inaweza kuwa ni vigumu sana kwa mtu yeyote kujifunza.
 • Kumtunza mtu mwengine na kusaidiana. Kuwa mwenye huruma kwa kila mmoja, hasa wakati wa matatizo.
 • Matunzo hufanyika kwa kila mtu. Watu wazima hutunza watoto, watoto hujali watu wazima, watu wazima hutunza watu wazima na watoto hujali watoto.
 • Kila mtu hujifunza na kuiga tabia za watu wanaomzunguka. Onesha tabia unayotaka kuiona.

Additional information

Weight 0.045 kg
Dimensions 0.3 × 21 × 29.7 cm

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Home learning (Swahili)”

Your email address will not be published.